Smartdesmarttz: HABARI ZA KITAIFA

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI ZA KITAIFA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI ZA KITAIFA. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 12 Agosti 2018

HII NDIYO SABABU YA WASAFI TV,CLOUDS TV,CHANNEL TEN,STAR TV KUTO KUONEKANA KATIKA VING'AMUZI KAMA Dstv,AZAM TV

Jumapili, Agosti 12, 2018 0
HII NDIYO SABABU YA WASAFI TV,CLOUDS TV,CHANNEL TEN,STAR TV KUTO KUONEKANA KATIKA VING'AMUZI KAMA Dstv,AZAM TV


SERIKALI imewataka watoa huduma wa ving’amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku wazingatie sheria na kanuni kwa kutorusha maudhui ya televisheni ambayo hayamo kwenye leseni zao za biashara. Hatua hiyo ya serikali imekuja baada ya huduma za utangazaji wa maudhui za Channel Ten, ITV, Star Tv, EATV na Clouds Tv kusitishwa kwenye king’amuzi cha Azam kwa mujibu wa tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) la Agosti 7, mwaka huu. TCRA ilitangaza hivi karibuni kupitia vyombo vya habari kusudio la kuzifunga leseni za kampuni ya Multichoice, Zuku na Azam endapo wataendelea kuonesha maudhui ya chaneli hizo za televisheni kwa watazamaji kwa vile ni kinyume cha sheria na kanuni za leseni zao. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema Agosti 11 mwaka huu, vituo vya ITV, Clouds Tv, EATV na Channel Ten walitoa tamko lao kupitia mitandao ya kijamii vikitaka busara iliyotumika awali kwa vituo hivyo kupeleka maudhui yao kupitia ving’amuzi vya Zuku, Azam na Multichoice kinyume na sheria, iendelee wakati utaratibu wa kurekebisha hali hiyo ukiendelea. Kamwelwe alisema hoja hiyo imepingwa na serikali kwa kuwa TCRA haiwezi kukaa kimya huku sheria na kanuni za utangazaji zikivunjwa na watoa huduma hao. “Watoa huduma hao Azam, Multichoice na Zuku waliamua kwenda Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya TCRA, lakini Mahakama Kuu ilitupilia mbali pingamizi hilo la Agosti 22, 2017,” alieleza Kamwelwe. Kwa mujibu wa Kamwelwe, leseni namba moja ya vituo vya televisheni nchini inawataka kutoa matangazo yao ikiwemo habari, sherehe za kitaifa, matukio ya magonjwa, vipindi vya watoto na sherehe za kitaifa bure bila kuwataka wananchi kulipia huduma hizo. Amesema huduma binafsi kama vile mchezo wa mpira kwenye nchi za nje pamoja na tamthiliya ni michezo binafsi ambayo mwananchi kwa ridhaa yake anaweza kulipia ili aone. Baada ya kadhia hiyo, Kamwelwe alisema endapo watoa huduma hao, hawataendelea kutoa huduma wanazotakiwa kisheria kwa mujibu wa leseni zao, serikali itato tamko la kuwataka wawafidie wananchi ambao ni wateja wao


TAZAMA VIDEO HAPA CHINI


Jumatatu, 14 Mei 2018

MTANZANIA EBORA IMEINGIA,NJIA ZA KUZUIA , KWANINI EBORA INAKUJA MARA KWA MARA

Jumatatu, Mei 14, 2018 0
MTANZANIA EBORA IMEINGIA,NJIA ZA KUZUIA , KWANINI EBORA INAKUJA MARA KWA MARA

Virusi vya Ebola vimechomoza tena, mara hii katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Wakati ni vigumu kutabiri ni wapi au lini tena mlipuko huu unaweza kuzuka, ni wazi kuwa tunafahamu mengi sasa kuhusu namna ya kuzuia janga kutokea. Taarifa kuhusu kutokea mlipuko wa Ebola katika mji wa Bikoro kaskazini magharibi mwa Congo mara moja inaleta katika akili jinsi janga hilo linalotisha lililosababisha vifo vya watu 11,000 na wengine 28,000 kuambukizwa katika eneo la Afrika magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016. Ni jinamizi ambalo hakuna anayetaka kulishuhudia au kulipitia tena. Watu 600 watoweka kufuatia maporomoko Sierra Leone Maisha baada ya janga la Ebola Afrika Magharibi Tangu Aprili 4 nchini Congo, kumeripotiwa zaidi ya visa 30 ambavyo huenda ni vya ugonjwa wa Ebola - ikiwemo vifo vya watu 18 - licha ya kwamba ni visa viwili tu vilivyothibitishwa kutokana na Ebola. Basi ni kwanini Ebola hurudi mara kwa mara na ni jitihada gani zinazochukuliwa kuzuiwa kurudi upya kwa janga lililoshuhudiwa Afrika magharibi? Hauwezi kudhibitiwa Ebola unaweza kusambaa kwa kasi kupitia kugusa maji maji ya kutoka mwilini mwa muathiriwa. Dalili za kwanza zinazokuja kwa mfano wa homa sio rahisi kuzitambua. Janga la Afrika magharibi mnamo 2014-16 lilizuka katika kijiji kimoja cha mpakani nchini Guinea, na muathiriwa wa kwanza anadhaniwa kuwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili aliyefariki duniani mnamo 2013. Haki miliki ya pichaGOOGLE Image caption Mlipuko wa mwisho wa Ebola mnamo 2017 ni mojawapo ya milipuko 9 iliyoshuhudiwa DR Congo Ugonjwa huo ulisambaa nchini Guinea na nchi jirani Sierra Leone na Liberia, na kupindukia ulipofika maeneo ya mijini. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ipo maelfu ya maili kutoka mataifa ya Afrika magharibi yalioathirika na janga hilo. Kwamba janga hilo limezuka upya katika eneo la mbali sio jambo la kushangaza. Virusi vya Ebola vimegunduliwa katika miaka ya nyuma mnamo 1976 katika milipuko miwili ambapo watu 151 walifariki katika enoe la Nzara, Sudan kusini na watu 280 waliofariki katika eneo la Yambuku karibu na mto Ebola uliopewa jina kutokana na ugonjwa huo. Haki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY Image caption Virusi vya Ebola katika seli iliyoathirika Mlipuko huu wa sasa unafuatia mingine 8 iliyoshuhudiwa DR Congo. Kwa jumla kumeshuhudiwa milipuko 24 - ukiongezwa na wa kati ya 2014 -16 katika Afrika magharibi na kati ikiwemo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Uganda, Sudan na Gabon. Wakati tunapoyatambua maeneo yalio katika hatari kubwa, itakuwa sio uhalisia kufikiria kuwa ugonjwa wa Ebola utawahi kuangamizwa kabisa na ni vigumu kujua ni wapi au lini mlipuko mwingine unaweza kuzuka. Kutafuta kupuguza maambukizi Tunaweza kuisitisha milipuko kuwa majanga na tunaweza kuboresha mbinu za kuwakinga raia. Hatua ya pamoja na iliyoratibiwa katika kukabiliana na ugonjwa huu inaweza kuhakikisha ugonjwa unadhibitiwa mapema, ili watu wachache iwezekanavyo waugue au wafariki. Haki miliki ya pichaAFP Image caption Maelfu walifariki wakati Ebola uliporipotiwa Afrika magharibi mnamo 2014-16 Ni muhimu kwanza kutambua aina ya virusi na kunakili uwezekano wa maambukizi mapya wakati mlipuko unaporitiwa. Wataalamu kwa mfano kwa mlipuko wa sasa Congo ni lazima watambue chanzo cha maambukizi haraka iwezekanavyo. Watataka kujua mgonjwa huyo amekuwa karibu na nani, na pia ni nani walikuwa karibu na watu hao. Hili ni jambo linalohitaji kufanywa haraka. Muuguzi afariki baada ya wauguzi kuogopa kumgusa Waathiriwa na wanaoshukiwa kuambukizwa watatibiwa katika taasisi za afya katika eneo hilo. Hatua za usafi ni muhimu - ikiwemo kufuniko nyuso, na kuvaa magauni na glavu za mikono kuzuia mwili kugusa maji maji ya aina yoyote kutoka kwa muathiriwa. Chanjo zimekusanywa Kuna aina tano ya virusi vilivyotambuliwa vya Ebola, na kilicho hatari zaidi ni kile cha Zaire. Na ndicho kirusi kilichotambuliwa katika mlipuko wa sasa huko Congo ambapo sasa kuna chanjo ilio tayari kwa matumizi ya dharura. Haki miliki ya pichaCENTERS FOR DISEASE CONTROL AND

TAADHARI KWA WAKAZI WA DAR ES SAALAM

Jumatatu, Mei 14, 2018 0
TAADHARI KWA WAKAZI WA DAR ES SAALAM

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa kwa siku tano kuanzia jana, ambazo zinaweza kuleta mafuriko katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba. Katika taarifa ya TMA iliyotolewa jana Mei 13, mvua hizo zilizoanza kunyesha zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu. TMA imesema athari zinazinaweza kutokea ikiwemo mafuriko ambayo yanaweza kusababisha kuvurugika kwa usafiri, barabara kubwa kutopitika na maisha ya watu kuwa hatarini kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi. Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa.

Alhamisi, 10 Mei 2018

RAISI MAGUFULI AMTOA SUGU JELA

Alhamisi, Mei 10, 2018 0
RAISI MAGUFULI AMTOA SUGU JELA


JESHI la Magereza nchini limesema kuwa, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kwa msamaha wa Dkt. Rais John Magufuli alioutoa kwa wafungwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika Aprili 26, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Ofisa habari wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje, amesema katika maadhimisho hayo, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 3,319, kati yao wafungwa 585 waliachiliwa huru Aprili 26, 2018. Aidha, kwa mujibu wa sheria, Rais alipunguza moja ya tatu ya vifungo vya watuhumiwa mbalimbali walioko magerezani. “Mbali na hao, wafungwa wengine 2,734 waliendelea kubaki magerezani akiwemo Sugu na Masonga ili kumalizia sehemu ya kifungo kilichokuwa kimebaki baada ya kupewa msamaha huo na Rais Magufuli,” amesema Mboje. Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Jumapili, 6 Mei 2018

MTIHANI WA KIDATO CHA SITA KUANZA KESHO

Jumapili, Mei 06, 2018 0
MTIHANI WA KIDATO CHA SITA KUANZA KESHO
 


Katibu Mtendaji wa Balaza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles E. Msonde. KATIBU MTENDAJI wa Balaza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles E. Msonde leo ameongea na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema mitiani ya kidato cha sita (ACSEE) na Ualimu itafanyika tarehe 7 hadi 25 Mei 2018 katika jumla ya Shule za Sekondari 674, Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 231 na Vyuo vya Ualimu 125 Tanzania Bara na Zanzibar.

Ijumaa, 4 Mei 2018

BORA NINYWE SUMU LAKINI SIYO FEDHA ZA WANANCHI, ACHENII KUPOTOSHA WANANCHI

Ijumaa, Mei 04, 2018 0
BORA NINYWE SUMU LAKINI SIYO FEDHA ZA WANANCHI, ACHENII KUPOTOSHA WANANCHI


Rais Magufuli leo Ijumaa ameweka jiwe la msingi la Barabara ya Kidatu – Ifakara. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Wabunge wote wa Chadema na CCM mkoani Morogoro. Moja ya kauli ambazo Rais amezungumza leo; “Kuna maeneo ambayo wakandarasi wamekula hela za miradi, wamekula sumu. Hela ya Serikali ya awamu ya tano hailiwi bora ule sumu kali. Waliokula fedha waanze kujiandaa, kurudisha fedha na kutekeleza miradi au kukumbana na sheria ya mwaka 97.”



“Haiwezekani mimi nitafute hela halafu wewe uzile tu nikwambie umeula wa chuya. Kama makandarasi watakuwa wamekimbia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, polisi na Takukuru wawatafute popote. Watazitapika hizo fedha wanazozitafuna,” amesisitiza Rais. Amesema hatojali fisadi ametoka CCM, Chadema wala CUF au nje ya nchi, atawashughulikia.



Mbunge wa Kilombero, Lijualikali(CHADEMA) “Ukiniambia leo uwape zawadi gani watu wa Morogoro maana kuna mengi lakini naomba watu wote ambao wamechukua ardhi yetu na hawaifanyii kazi basi naomba leo uondoke nao kwa sababu watu hao wanahujumu rasilimali yetu na hii barabara kama tutaacha hivi basi kwetu itakuwa haina faida na mimi kama Mbunge nilikuwa nawaambia wananchi wangu msiuze ardhi hovyo kwani ardhi ndiyo rasilimali yetu” “Wananchi wana shida ya kujua wingi wa sukari, wanashida ya kujua ni namna gani uzito wa mua unapatikana kwani kiwanda ndiyo kinapima chenyewe uzito, kiwanda kinapima chenyewe wingi wa sukari wananchi wanapewa tu hesabu sasa hatuwezi kujua tunaibiwa au tuko sahihi” Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule(Prof. Jay) Profesa Jay amemuomba Rais Magufuli amsadie shilingi bilioni mbili ili kukamilisha mradi mkubwa wa maji uliopo katika Kata ya Ruaha. Pia amemuomba Rais kutatua changamoto nyingi zinalolikabili jimbo lake ikiwemo uboreshaji wa miundombinu.

MWENDOKASI INASIKITISHA!!

Ijumaa, Mei 04, 2018 0
MWENDOKASI INASIKITISHA!!


KAMPUNI inayotoa huduma katika mradi wa usafiei wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imsitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia leo saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa ambaye amesema UDART wameamua hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.




“Huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi – Kimara, Kimara – Morroco, Kimara – Magomeni Mapipa, Kivukoni – Muhimbili, Gerezani – Kvukoni na Gerezani – Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa”, amesema Bugaywa. Aidha, Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama nyingine.


Alhamisi, 3 Mei 2018

Ajipeleka polisi baada ya mzigo alioiba kunasa mabegani.

Alhamisi, Mei 03, 2018 0
Ajipeleka polisi baada ya mzigo alioiba kunasa mabegani.


Kijana Frank Japhet (23), mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, amelazimika kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania mabegani. Wakati akihojiwa kituoni hapo, mtuhumuwa huyo amesema mzigo huo, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Mei 3, 2018, akaongeza kwamba aliondoka na mzigo huo hadi eneo la Stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, ambapo mzigo huo uling’ang’ania kichwani. Ameendelea kusema kwamba alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi. Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shanna amesema walilazimika kumtafuta mhusika wa mzigo huo ili kuweza kumsaidia kijana Frank Joseph ambaye aliiba kiroba hicho, baada ya wao kushindwa kumtua.Kamanda Shanna ameendelea kusimulia kuwa wakati wakijaribu kumtua kijana huyo kiroba cha mahindi alichoiba alikuwa akilalamika kupata maumivu makali, na ndipo wakamsaka mmiliki wa mzigo ili kumsaidia.