RAISI MAGUFULI AMTOA SUGU JELA - Smartdesmarttz

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Alhamisi, 10 Mei 2018

RAISI MAGUFULI AMTOA SUGU JELA



JESHI la Magereza nchini limesema kuwa, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kwa msamaha wa Dkt. Rais John Magufuli alioutoa kwa wafungwa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika Aprili 26, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Ofisa habari wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje, amesema katika maadhimisho hayo, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 3,319, kati yao wafungwa 585 waliachiliwa huru Aprili 26, 2018. Aidha, kwa mujibu wa sheria, Rais alipunguza moja ya tatu ya vifungo vya watuhumiwa mbalimbali walioko magerezani. “Mbali na hao, wafungwa wengine 2,734 waliendelea kubaki magerezani akiwemo Sugu na Masonga ili kumalizia sehemu ya kifungo kilichokuwa kimebaki baada ya kupewa msamaha huo na Rais Magufuli,” amesema Mboje. Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni