MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ leo Agost 9, 2018. Mzee King Majuto alifariki dunia jana majira ya saa 2:00 usiku Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Baada ya kuaga mwili utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa. Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI ZA MASTAA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI ZA MASTAA. Onyesha machapisho yote
Alhamisi, 9 Agosti 2018
DUH KALALE MAHARAPEMA BABU YETU (NEVER SEE U AGAIN)
Smartdesmart
Alhamisi, Agosti 09, 2018
0
MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ leo Agost 9, 2018. Mzee King Majuto alifariki dunia jana majira ya saa 2:00 usiku Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Baada ya kuaga mwili utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa. Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
Jumatano, 8 Agosti 2018
MZEE MAJUTO 😭😭😭 AMEFARIKI DUNIA LEO TAREHE 8/08/2018 CHANZO CHA KIFO CHAKE NI
Smartdesmart
Jumatano, Agosti 08, 2018
0
MSANII nguli wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman ‘Mzee King Majuto’ amefariki dunia majira ya saa 2:00 usiku huu wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Mtoto wa marehemu aitwaye Abuu amethibitisha kifo cha baba yake. Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram. “R.I.P King Majuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana katika Tasnia ya Comedy Tanzania, sisi wanao, tutakukumbuka kwa kazi zako, upendo wako, tabasamu lako Daima milele, tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani Mzee wetu,” amendika Joti. Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma Shule Msambwini, mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10. Hivi karibuni Mzee Majuto alisafirishwa na kupelekwa nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejea nchini ambapo alipelekwa Muhimbili kuendelea na tiba yake. Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali. “Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un, We belong to God and to Him we shall return.”
Alhamisi, 7 Juni 2018
ALIKIBA ATANGAZA KIKOSI CHAKE RASMI LEO
Smartdesmart
Alhamisi, Juni 07, 2018
0
Mwanamuziki, Alikiba ametangaza kikosi chake kitakachocheza mchezo wa hisani utakaochezwa Jumamosi kati na marafiki zake na marafiki wa Mbwana Samatta. Kiba alisisitiza kuwa wameamua kuungana vijana kwa pamoja kwa ajili ya kufanya kitu kwenye sekta ya elimu. “Kutokana na kutambua umuhimu wa elimu nchini ndio maama tumejitolea kuwa mabalozi ambao tutahamasisha kuchangia vifaa vya kujifunzia na kufundishia na uimarishaji wa miundombinu,” alisema Alikiba. Nyota wa kikosi cha marafiki wa Kiba ni Shaaban Kado, Aishi Manula, Gadiel Michael, Said Ndemla, Adam Salamba, Paul Nonga, Abdul Kiba, Himid Mao, Erasto Nyoni, Agrey Morris, Ibrahim Ajib. Wengine ni Haruna Niyonzima, Abdi Kassim, Emmanuel Okwi, Abdi Banda, Saimon Msuva, Shaban Kisiga, Uhuru Seleman na Ramadhani Chombo. Nyota wa timu Samatta ni Juma Kaseja, Kabaly Faraji, Shomari Kapombe, Mohammedi Zimbwe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Athumani Chuji, Haruna Shamte, Mohammed Samatta. Wengine ni Tresor Mputu, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa, Haruna Moshi ‘Boban’, Amri Kiemba, Athuman Machupa, Henry Joseph, Rashid Gumbo, Mrisho Ngassa na Sultan Kaskas. Viingilio kwenye mchezo huo utakaochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Sh2000 kwa mzunguko huku jukwaa maalum ‘VIP’ ikiwa ni buku tatu Sh3000.
Jumamosi, 26 Mei 2018
qchila. aghairi kuacha mziki,apata mdhamini
Smartdesmart
Jumamosi, Mei 26, 2018
0
Mwanamuziki aliyewahi kutamba na nyimbo za Uhali Gani, Si Ulinikataa, Nikilala Naota na nyingine nyingi, Q Chillah ameghairi kuachana na muziki kama alivyotangaza awali baada ya kupata mfadhili aliyetangaza kuwa atamsaidia kumrudisha kwenye chati. Chillah amesema alikusudia kuachana na muziki kwa sababu alipotezewa na wadau wa muziki akidai kuwa wapo wengine walikosea, lakini walirudishwa katika mstari akimtolea mfano Saida Karoli na Ruby ambao sasa wanafanya vizuri. Akizungumzia sababu ya kusikitisha uamuzi huo mzito anasema: “Niliona nakuwa mtumwa wa makosa yangu nikaona bora niutue mzigo huu, nikiwatazama watoto wangu nilijiona na madeni, sipo kwenye dunia ambayo wenzangu wapo.” Hata hivyo uamuzi huo ulifikia tamati baada ya kuaminishwa kuwa tasnia bado inamhitaji, hivyo alibadili uamuzi wake. “Tangu nimetangaza kuacha muziki, nimeona mapenzi ya Watanzania, nimeona mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio ‘support’ yao, labda ni mimi au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu.”
Jumatatu, 14 Mei 2018
KILICHO SABABISHA WEMA KUTO TOKEA KWENYE UZINDUZI WA YA AUNT EZEKIEL
Smartdesmart
Jumatatu, Mei 14, 2018
0
Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza sababu ya kushindwa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu fupi ya dakika 20 ‘MAMA’ ya Aunt Ezekiel iliyofanyika usiku wa jana (Jumapili) Mlimani City jijini Dar es Salaam. Madam Sepenga ametoa taarifa hiyo kupitia kwenye mtandao wa Instagram akidai kuwa alichelewa kutokana na Mama yake ndio alimchelewesha na kujikuta ameshindwa kufika kwenye uzinduzi huo. “I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…😩😩😩,” ameandika Wema kwenye mtandao huo. Hata hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.
Lulu arejeshwa nyumbani kwa amri maalumu
Smartdesmart
Jumatatu, Mei 14, 2018
0
Dar es Salaam. Mcheza Filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu amebadilishiwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’. Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Akizungumza na MCL Digital Jumatatu Mei 14, 2018, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam. “Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje

