qchila. aghairi kuacha mziki,apata mdhamini - Smartdesmarttz

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Jumamosi, 26 Mei 2018

qchila. aghairi kuacha mziki,apata mdhamini


Mwanamuziki aliyewahi kutamba na nyimbo za Uhali Gani, Si Ulinikataa, Nikilala Naota na nyingine nyingi, Q Chillah ameghairi kuachana na muziki kama alivyotangaza awali baada ya kupata mfadhili aliyetangaza kuwa atamsaidia kumrudisha kwenye chati. Chillah amesema alikusudia kuachana na muziki kwa sababu alipotezewa na wadau wa muziki akidai kuwa wapo wengine walikosea, lakini walirudishwa katika mstari akimtolea mfano Saida Karoli na Ruby ambao sasa wanafanya vizuri. Akizungumzia sababu ya kusikitisha uamuzi huo mzito anasema: “Niliona nakuwa mtumwa wa makosa yangu nikaona bora niutue mzigo huu, nikiwatazama watoto wangu nilijiona na madeni, sipo kwenye dunia ambayo wenzangu wapo.” Hata hivyo uamuzi huo ulifikia tamati baada ya kuaminishwa kuwa tasnia bado inamhitaji, hivyo alibadili uamuzi wake. “Tangu nimetangaza kuacha muziki, nimeona mapenzi ya Watanzania, nimeona mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio ‘support’ yao, labda ni mimi au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni