MSANII nguli wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman ‘Mzee King Majuto’ amefariki dunia majira ya saa 2:00 usiku huu wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Mtoto wa marehemu aitwaye Abuu amethibitisha kifo cha baba yake. Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram. “R.I.P King Majuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana katika Tasnia ya Comedy Tanzania, sisi wanao, tutakukumbuka kwa kazi zako, upendo wako, tabasamu lako Daima milele, tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani Mzee wetu,” amendika Joti. Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma Shule Msambwini, mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10. Hivi karibuni Mzee Majuto alisafirishwa na kupelekwa nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejea nchini ambapo alipelekwa Muhimbili kuendelea na tiba yake. Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali. “Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un, We belong to God and to Him we shall return.”
Jumatano, 8 Agosti 2018
Home
HABARI ZA MASTAA
MZEE MAJUTO ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ AMEFARIKI DUNIA LEO TAREHE 8/08/2018 CHANZO CHA KIFO CHAKE NI

Tags
# HABARI ZA MASTAA
About Smartdesmart
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of soratemplates is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
HABARI ZA MASTAA
Lebo:
HABARI ZA MASTAA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni