WEMA SEPETU, AJATOLEA KULEA YATIMA - Smartdesmarttz

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Ijumaa, 4 Mei 2018

WEMA SEPETU, AJATOLEA KULEA YATIMA



MWANADADA kipenzi cha mashabiki wa Filamu za Bongo, Wema Sepetu amesema wakati nyota wenzake wanapenda starehe za dunia yeye furaha yake kubwa ni kuona watoto yatima wanapata mahitaji yao muda muafaka, halafu mambo mengine yanafuata. Wema alilitonya Mwanaspoti kuwa, watu wanadhani yeye ni mtu wa starehe kwa namna wanavyomuona, lakini ukweli ni kwamba, starehe yake kubwa ni kuwaona watoto yatima mara kwa mara, na ndio maana kila wakati anaenda kuwapa msaada katika vituo vyaoo. “Naguswa sana na watoto hawa, hivyo nimejiwekea ratiba kila mwisho wa mwezi au katikati ya mwezi naenda kuwatembelea na kuwasaidia baadhi ya changamoto walizonazo. Asikwambie mtu hawa watoto yatima wana baraka zote kutoka kwa Mwenyezi Mungu,” alisema Wema. Mrembo huyo wa mwaka 2006 alisema, suala la kusaidia liko moyoni mwake kwani hata kwa watu wake wa karibu huwa anawasaidia sana lakini matokeo yake wanamgeuka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni