Hata hivyo, haikufahamika mapema sababu za mastaa hao ambao, wote ni wa kikosi cha kwanza na wachezaji muhimu wenye uwezo wa kuamua mechi ndani ya dakika 90 za mchezo.
BADO kuna wingu pale Jangwani, Yanga imepaa jana alasiri kwenda jijini Algers nchini Algeria, lakini ikilazimika kuwaacha nyuma mastaa wake wanne ambao hawakuwepo kwenye msafara huo. Hata hivyo, haikufahamika mapema sababu za mastaa hao ambao, wote ni wa kikosi cha kwanza na wachezaji muhimu wenye uwezo wa kuamua mechi ndani ya dakika 90 za mchezo. Mwanaspoti ambalo limeshatua kule jijini Algers mapema kabisa kuwasubiri Yanga, lakini wakati ikiondoka jana mastaa wake Kelvin Yondani, ambaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana kwa kosa la kumtemea mate beki wa Simba, Asante Kwasi, hakuwepo kwenye msafara. Mbali na Yondani, wengine ambao hawakuwepo kwenye safari hiyo ni kiungo fundi wa mpira, Pappy Kabamba Tshishimbi, Thabani Kamusoko na washambuliaji Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa. Akizungumza na Mwanaspoti kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere jana, Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, alieleza kushangazwa kwake na kutowaona wachezaji kwenye safari hiyo. Alisema mchezo dhidi ya Waarabu hao ni mgumu na kwamba, kikosi chake kinakwenda kupambana kupata matokeo mazuri ili kujiweka mahali pazuri kwenye msimamo wa Kundi D ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika. Hata hivyo, Zahera alisema alilazimika kuulizia walipo wachezaji hao, lakini majibu hayakuwa mazuri kwani kila mmoja alielezwa kuwa na tatizo tofauti. Imeelezwa kuwa, Chirwa na Tshishimbi na Ajib haikufahamika sababu za kushindwa kuwa kambini kama walivyotangaziwa awali. Kwa upande wa Yondani, Zahera alisema kilichomchanganya ni kusikia beki huyo kisiki na mahodha msaidizi amezima simu yake ya kiganjani na hakuna kiongozi aliyefanikiwa kumpata wakati wakimtafuta ili kufahamu sababu ya kutofika kambini. “Nimeshtuka na kushangazwa sana na kutowaona wachezaji wangu ambao, ni muhimu uwanjani na walipaswa kuwepo. Tuna mechi ngumu na lazima tuwe jeshi kamili ili kuwakabili wapinzani wetu. Kuwakosa wachezaji hawa ni pigo kubwa na nilipojaribu kuuliza nikaambiwa Kelvin amezima simu, lakini wengine hawakufika kambini,” alisema Zahera na kuongeza kuwa: Chirwa ni majeruhi ila hajafika kambini na Kamusoko nimeambiwa pasi yake ya kusafiria ina matatizo.” Kukaa jukwaani, simu kutumika Zahera yuko sambamba na jeshi lake kwenye safari ya Algeria, lakini habari mbaya ni kuwa hataweza kukaa kwenye benchi la ufundi kutoa maelekezo. Kocha huyo bado hajakamilisha taratibu za kukalia benchi la Yanga, lakini mabosi wake wamefanya mchakato kuhakikisha anakuwa na mawasiliano ya uhakika na makocha wasaidizi. Habari zinaeleza kuwa, katika mchezo dhidi ya Simba kulikuwa na dosari kwenye mabadiliko ya wachezaji na sasa hawataki hilo litokee tena na kuamua kufanya jambo la maana. “Tunataka kuona kocha anakuwa na mawasiliano ya haraka pale uwanjani, hii ni mechi ngumu sana, unajua katika mchezo wa Simba kuna makosa yalifanyika kwenye sub na hatutaki yatokee,” alisema mmoja wa mabosi wa Yanga. “Kuna vifaa kocha ametuelekeza tutavitafuta kule Algeria ili aweze kuwasiliana na akina Nsajigwa (Shadrack) akiwa jukwaani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni