WACHEZAJI WA YANGA WAMEWEKA MGOMO,LICHA YA KUKANUSHWA NA MSEMAJI WA YANGA - Smartdesmarttz

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Jumamosi, 5 Mei 2018

WACHEZAJI WA YANGA WAMEWEKA MGOMO,LICHA YA KUKANUSHWA NA MSEMAJI WA YANGA



YANGA imeshatua Algeria tangu jana Ijumaa tayari kuivaa USM Alger, lakini huku Tanzania iliacha mshtuko kutokana na baadhi ya mastaa wake muhimu wa kikosi cha kwanza kushindwa kusafiri. Hata hivyo, mabosi wa Yanga kuanzia juzi walikuwa wakihaha kutafuta mawasiliano na wachezaji hao waliobaki nyuma na kiasi cha kuwatisha mashabiki wao, lakini hatimaye Mwanaspoti limenasa ukweli mzima. Yanga wakati ikipaa juzi jioni katika hali iliyoshtua na kumpagawisha kocha mpya, Mkongo Mwinyi Zahera ni kubaki kwa mabeki Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, viungo Pappy Kabamba Tshishimbi, Thabani Kamusoko na washambuliaji Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa. Kuanzia muda huo mabosi wa Yanga hawakutaka kulala na kuanza kuwasaka mmoja baada ya mwingine na wa kwanza kupatikana alikuwa Ajibu ambaye kumbe tatizo ni mkewe anayekaribia kujifungua hivyo, kuhitaji uangalizi wa karibu. AJIBU Taarifa zinaeleza baada ya Ajibu kupatikana mabosi hao waliweka mipango sawa ya kumpandisha ndege kwenda kuungana na wenzake, lakini dili hilo lilikwama jana baada ya daktari wa mkewe kutaka mgonjwa huyo kupatiwa uangalizi maalumu huku Ajibu akitakiwa kila wakati kutoa taarifa za maendeleo ya mkewe kwa kadiri mambo yanavyobadilika. Jambo hilo likachukuliwa kwa uzito mkubwa na mabosi wa Yanga na wakalazimika kubadili gia ngani na kumwacha staa wao huyo waliyemnasa kutoka Simba, kubaki jijini ili kutoa uangalizi wa karibu kwa mkewe aweze kujifungua salama. Tshishimbi Unapolitaja jina la kiungo wa nguvu ndani ya Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi basi mashabiki wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara hubaki na tabasamu tu. Ndio! Huduma ya Tshishimbi klabuni Yanga si ya kitoto kabisa tangu alipowasili na kutoonekana kwake kwenye safari hiyo kuliwavuruga wengi vichwa, lakini kumbe kuna siri imejificha nyuma yake. Taarifa zinaeleza kwamba Tshishimbi hakuwa kwenye hesabu za kusafiri baada ya kugundulika kuwa ni majeruhi na asingeweza kucheza mchezo huo dhidi ya Waarabu hao. Tshishimbi aliumia kabla ya mchezo wa Mbeya City, lakini jeraha hilo liliongezeka wakati wa mchezo dhidi ya Simba wakati nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni mgonjwa akisumbuliwa na malaria tangu wakati Yanga ikijiandaa kuikabili Simba. Katika msafara wa wachezaji 19 ambao waliondoka juzi kwenda Algeria, Tshishimbi hakuwemo kabisa na hakuna taratibu zozote za safari zilizofanyika. Jana, wakati wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakipambana na mvua kiungo huyo alikuwa kwa mtaalamu akipatiwa matibabu ya jeraha hilo. Kamusoko Mzimbambwe huyo kwa muda mrefu alikuwa majeruhi, lakini hivi karibuni alianza kurudi uwanjani. Hata hivyo, hakuweza kuungana na wenzake kwenye safari hiyo kutokana na kukosa nyaraka muhimu ikiwemo kunyimwa visa ya kuingia Algeria kufuatia kibali chake cha kazi nchini kufikia tamati. Mabosi wa Yanga tayari wameanza mchakato wa kumtafutia vibali vingine, lakini havijaweza kukamilika kwa wakati kumwezesha kusafiri na wenzake. Chirwa Kwenye msako wa Mzambia, Obrey Chirwa kulikuwa na mtihani kidogo ambapo, inaelezwa kuwa anasumbuliwa na malaria. Jana mchana Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alieleza kuwa, Chirwa anasumbuliwa na malaria hivyo, hakuweza kusafiri na kikosi kwenda kucheza mchezo huo muhimu. Lakini, Mwanaspoti linafahamu kuwa nidhamu ya straika huyo imeanza kuwachosha mabosi zake kutokana na kusumbua mara kwa mara. Imeelezwa kuwa Chirwa amekuwa akidengua kwa madai ya kudai stahiki zake huku ikiaminika kwamba amekuwa akipigiwa hesabu kali kuhusiana na hatma yake klabuni hapo. Yondani Mashabiki wa Yanga wana uhakika wa kupata huduma bora ya kulindiwa goli lao pindi wanapomuona nahodha msaidizi, Kelvin Yondani pale nyuma akiunda ukuta wa nguvu na Andrew Vincent (Dante) na Ninja. Yaani mashabiki wa Yanga kwa huyu Yondani huwaelezi kitu unaambiwa, lakini safari hii sio mashabiki wala mabosi wanaofahamu beki huyu kisiki mahali alipo. Jana, mabosi wa Yanga walifanya msako wa maana tu kumtafuta Yondani, ambaye juzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni