OKWI APEWA KIATU CHA DHAABU KABLA YA LIGI KUISHA - Smartdesmarttz

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Jumamosi, 5 Mei 2018

OKWI APEWA KIATU CHA DHAABU KABLA YA LIGI KUISHA



HATIMAYE jamaa wamekubali kuwa straika wa Simba, Emmanuel Okwi, ni hatari na anastahili kupewa tuzo yake ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu. Okwi anaongoza akiwa na mabao 19 mpaka sasa akifuatiwa kwa mbali na pacha wake, John Bocco ambaye ana mabao 14. Straika wa Mbeya City, Eliud Ambokile, mwenye mabao 9 amesema Okwi ana kasi kubwa ya kuzifumania nyavu hivyo, anaamini ndiye atachukua Kiatu cha Dhahabu. “Bila kupepesa macho nimesalenda na kumpa asilimia kubwa Okwi kubeba tuzo msimu huu, ametuacha mbali sana na ukitazama anavyocheza hawezi kupitwa tena,” alisema. “Malengo yangu ni kumaliza msimu nikiwa na mabao 16, siwezi kuingia kwenye mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu kwa sasa, kiuhalisia ni ngumu na kwa Okwi njia ni wazi kwake.” Nyota mwingine aliyempa kura Okwi ya kuwa mfungaji bora kwa msimu huu ni Khamis Mcha wa Ruvu Shooting, aliyedai straika huyo yupo kwenye moto kweli kweli katika kufumania nyavu. “Kiukweli Okwi msimu huu yupo vizuri, ana asilimia kubwa ya kuchukua kiatu cha ufungaji bora, kiwango chake kipo juu na timu inamwezesha kufikia malengo yake,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni