Mbeya. Yametimia, Yanga imevuliwa ubingwa rasmi baada ya kukubalia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Matokeo hayo yanaifanya Simba kuchukua bingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza tangu 2011-12, bila ya kucheza mechi yake dhidi ya Singida United. Yanga imebaki nafasi ya tatu na pointi zake 48, na hata kama itashinda mechi zake zote zilizobaki itafikisha pointi 63, wakati Simba ikiongoza ligi kwa pointi 65 na Azam ya pili pointi 49. Prisons ilipata bao la kwanza dakika 57, kwa mkwaju wa penalti wa Eliuter Mpeto kabla ya Salum Bosco kufunga bao pili dakika 85, kwa kuwapiga chenga kipa na mabeki wa Yanga kabla ya kufunga. Yanga iliyokwenda kwenye mchezo huo ikiwa na kikosi dhaifu baada ya kocha wake Mkongo Mwinyi Zahera kushauri kuigawa timu hiyo na nyingine ibaki Dar es Salaam ikijianda na mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports. Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya Prison ni kipa ni Beno Kakolanya, Juma Abdul, Emmanuel Martin, Pato Ngonyani na Abdallah Shaibu 'Ninja'. Viungo ni Maka Edward na Thabani Kamusoka, Paulo Godfrey na Barnan Akilimali huku washambuliaji Yohana Mkomola na Matheo Anthony. Benchi la ufundi la Yanga liliongozwa na kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa pekee.
Alhamisi, 10 Mei 2018
YANGA INASIKITISHA IMESHINDWA KUTETEA UBINGWA!!!

Tags
# MICHEZO
About Smartdesmart
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of soratemplates is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
MICHEZO
Lebo:
MICHEZO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni