NGASSA: SIMBA WAPEWE KOMBE LEO!!! - Smartdesmarttz

BELIEVE WHAT YOU HAVE(MWANZO MGUMU)

Jumanne, 8 Mei 2018

NGASSA: SIMBA WAPEWE KOMBE LEO!!!



Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amekiri Simba wanastahili kuwa mabingwa kutokana na kiwango chao cha hali juu msimu huu. Simba inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 65, ikifuatiwa na Azam (49) na Yanga (48) wakati ligi hiyo ikielekea mwishoni. Ngassa alisema tangu Simba wameanza ligi wamekuwa wakiongoza, hawajapoteza mechi yoyote na wameweza kupata pointi dhidi ya timu tatu za juu jambo ambalo lilikuwa ishara tosha msimu huu wapo vizuri. "Simba ina wachezaji wenye uwezo binafsi wa kuamua mechi ngumu, na ndio timu ambayo inaonekana kukamilika katika kila idara jambo ambalo usipowapa pongezi utakuwa si mtu wa mpira," alisema Ngassa aliyewahi kucheza Yanga na Azam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni