MATUMAINI ya mshambuliaji wa Difaa El Jadida, Saimon Msuva kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Morocco ‘Batola Pro. msimu huu yamepotea, baada ya kikosi chaop kufungwa mabao 3-1 na Hassania Agadir. Difaa imeshuka hadi nafasi ya tano kutokana na kipigo hicho ikisaliwa na pointi 45 walizozikusanya kwenye mechi 29, na sasa wamesaliwa na mchezo mmoja wa Batola Pro kabla ya msimu kumalizika. Akizungumzia kuukosa kwake ubingwa wa Batola Pro, Msuva alisema ugumu wa ratiba yao ndani ya mwezi Aprili hadi Mei, ulichangia kupoteza nafasi ya kuchukua ubingwa huo. Lakini, wanajipanga upya. “Kuna michezo karibu mitatu tumecheza na vigogo wa huku japo hiyo sio sababu ya msingi, lakini kwa kiasi fulani tulipoteza kasi kutokana na ugumu wa mechi hizo. “Mbele yetu tuna mchezo mmoja uliobaki kwa hiyo inatakiwa tushinde ili tumalize kwenye nafasi za kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani,” alisema Msuva. Kuhusu maandalizi yao ya mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika TP Mazembe ya DR Congo, Msuva alisema yamekamilika jana kwa kufanyia kazi namna ya kuwashambulia. Difaa ambayo ilitoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua hiyo ya makundi dhidi ya MC Algers ipo nafasi ya pili na pointi moja kwenye kundi B linaloongozwa na Mazembe wenye pointi tatu.
Jumatatu, 14 Mei 2018
MSUVA AFICHUA MAZITO YANGA

Tags
# MICHEZO
About Smartdesmart
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of soratemplates is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
MICHEZO
Lebo:
MICHEZO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni