Dar es Salaam. Wakazi wa nyumba 130 zilizopo kata za Kibada na Kisarawe II wilayani Kigamboni akiwamo msanii wa vichekesho Lucas Mhavile ‘Joti’ wameingia katika mgogoro na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), baada ya majengo yao kuwekwa alama za x na kutakiwa kubomolewa. Akizungumza jana,Mei 3, 2018 Ofisa Habari wa manispaa ya Kigamboni David Langa amesema hatua hiyo imesababisha wakazi hao kuwa na taharuki kwa sababu wanamiliki viwanja hivyo kihalali na kodi wanatoa. Langa amesema tatizo lililojitokeza ni Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi ilipopima maeneo hayo, Tanroad walikuwa bado hawajaweka alama zao za barabarani na viwanja hivyo ni vya muda mrefu na wamekuja kuweka wakati vimeshaendelezwa. Kutokana na sintofahamu hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa aliwataka wananchi wote waliowekewa alama hizo kufika ofisini kwake Mei 5 kwa ajili mazungumzo yatakayowakutanisha wataalamu wa wizara, Tanroads na Manispaa ili kuona namna bora ya kufikia muafaka wa sintofahamu hiyo. Nyumba za wakazi hao zinatakiwa kubomolewa ndani ya siku 90.“Ofisi yangu na wataalamu haipo tayari kuona watu wakionewa naomba mjitokeze siku ya Jumamosi,”amesema Mgandilwa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakazi eneo la Kibada.
Ijumaa, 4 Mei 2018
Msanii Joti na wananchi zaidi ya 120 kubomolewa nyumba zao Kigamboni.

Tags
# HABARI ZA MASTAA

About Smartdesmart
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of soratemplates is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
HABARI ZA MASTAA
Lebo:
HABARI ZA MASTAA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni