Jumanne, 14 Agosti 2018
NEW AUDIO (WCB) Diamond platnumz ft mbosso & lavalava - JIBEBE
Smartdesmart
Jumanne, Agosti 14, 2018
0
Jumapili, 12 Agosti 2018
HII NDIYO SABABU YA WASAFI TV,CLOUDS TV,CHANNEL TEN,STAR TV KUTO KUONEKANA KATIKA VING'AMUZI KAMA Dstv,AZAM TV
Smartdesmart
Jumapili, Agosti 12, 2018
0
SERIKALI imewataka watoa huduma wa ving’amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku wazingatie sheria na kanuni kwa kutorusha maudhui ya televisheni ambayo hayamo kwenye leseni zao za biashara. Hatua hiyo ya serikali imekuja baada ya huduma za utangazaji wa maudhui za Channel Ten, ITV, Star Tv, EATV na Clouds Tv kusitishwa kwenye king’amuzi cha Azam kwa mujibu wa tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) la Agosti 7, mwaka huu. TCRA ilitangaza hivi karibuni kupitia vyombo vya habari kusudio la kuzifunga leseni za kampuni ya Multichoice, Zuku na Azam endapo wataendelea kuonesha maudhui ya chaneli hizo za televisheni kwa watazamaji kwa vile ni kinyume cha sheria na kanuni za leseni zao. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema Agosti 11 mwaka huu, vituo vya ITV, Clouds Tv, EATV na Channel Ten walitoa tamko lao kupitia mitandao ya kijamii vikitaka busara iliyotumika awali kwa vituo hivyo kupeleka maudhui yao kupitia ving’amuzi vya Zuku, Azam na Multichoice kinyume na sheria, iendelee wakati utaratibu wa kurekebisha hali hiyo ukiendelea. Kamwelwe alisema hoja hiyo imepingwa na serikali kwa kuwa TCRA haiwezi kukaa kimya huku sheria na kanuni za utangazaji zikivunjwa na watoa huduma hao. “Watoa huduma hao Azam, Multichoice na Zuku waliamua kwenda Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya TCRA, lakini Mahakama Kuu ilitupilia mbali pingamizi hilo la Agosti 22, 2017,” alieleza Kamwelwe. Kwa mujibu wa Kamwelwe, leseni namba moja ya vituo vya televisheni nchini inawataka kutoa matangazo yao ikiwemo habari, sherehe za kitaifa, matukio ya magonjwa, vipindi vya watoto na sherehe za kitaifa bure bila kuwataka wananchi kulipia huduma hizo. Amesema huduma binafsi kama vile mchezo wa mpira kwenye nchi za nje pamoja na tamthiliya ni michezo binafsi ambayo mwananchi kwa ridhaa yake anaweza kulipia ili aone. Baada ya kadhia hiyo, Kamwelwe alisema endapo watoa huduma hao, hawataendelea kutoa huduma wanazotakiwa kisheria kwa mujibu wa leseni zao, serikali itato tamko la kuwataka wawafidie wananchi ambao ni wateja wao
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Jumamosi, 11 Agosti 2018
KOCHA WA MANCHSTER UNITED JOSE MOURINHO AMPA SIFA POGBA
Smartdesmart
Jumamosi, Agosti 11, 2018
0
Penalti ya kiufundi aliyoifunga akiupeleka mpira karibu na mwamba wa juu wakati kipa Kasper Schmeichel akianguka chini iliwainua vitii mashabiki wa United Manchester, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ni kama alimtia ndimu Paul Pogba baada ya kumpa unahodha kwenye mchezo wa juzi usiku wa ufunguzi wa Ligi Kuu England. Katika mchezo huo Pogba alifunga bao la kuongoza dakika ya tatu kwa mkwaju wa penalti, United ilipoifunga Leicester City kwa mabao 2-1 na kiungo huyo alikuwa kwenye kiwango cha juu sawa na kile alichokionyesha katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia. Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa Mourinho alitumia mbinu ya kumpa Pogba unahodha wa mchezo huo ili kumsukuma ajitume zaidi na hilo lilifanikiwa. Mourinho ambaye msimu uliopita alimlaumu mchezaji huyo mara kadhaa akimtuhumu kucheza chini ya kiwango, aliamua kutumia mbinu hiyo, kjuzima ule msuguano uliokuwapo hasa ikizingatiwa Pogba aliomba kuihama United ili ajiunge na Barcelona. Pogba ambaye alianza mazoezi na wenzake siku nne kabla ya mchezo huo, hivyo hakupaswa kucheza mchezo huo, lakini yeye mwenyewe akamuomba Kocha ampange na alicheza kwa kiwango cha juu sawa na alivyofanya kwenye fainali za Kombe la Dunia. Penalti ya kiufundi aliyoifunga akiupeleka mpira karibu na mwamba wa juu wakati kipa Kasper Schmeichel akianguka chini iliwainua vitii mashabiki wa United na penalti hiyo ilitokana na Daniel Amartey kuunawa mpira uliopigwa na Alexis Sanchez. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko, katika kipindi cha pili mlinzi wa pembeni kushoto Luke Shaw akaongeza la pili likiwa la kwanza kwake tangu apandishwe kucheza kikosi cha kwanza, alifunga kiustadi baada ya kupokea pande la Juan Mata. Bao la kufutia machozi la Leicester lilifungwa na mtokea benchi Jamie Vardy kwa kichwa akiunganisha krosi ya Ricardo Perreira iliyogonga mwamba na kurudi uwanjani kisha mfungaji akauwahina kuukwamisha wavuni. Tukio la kuvutia uwanjani lilikuja katika dakika za lala salama Leicester ilipopata kona na kipa Schmeichel aliliacha lango lake na kwenda mbele kusaidia kusaka bao la kusawazisha na nususra afunge bao lakini mpira aliopiga kichwa ulitoka sentimita chache. Pogba alipumzishwa katika dakika ya 84 nafasi yake ikichukuliwa na Marouane Fellaini, huku Mourinho akijitetea kumchezesha kwa dakika nyingi licha ya kutofanya mazoezi ya kutosha. "Tulipanga kumchezesha Pogba kwa angalau dakika 60 lakini akacheza zaidi ya dakika 80, kwa kuwa alionekana yupo fiti na alicheza kwa kiwango cha juu,” alisema Mourinho.
Ijumaa, 10 Agosti 2018
DOWNLOADING:Wimbo ulioimbwa kwajili ya mzee majuto(lakini haina jinsi ni kazi ya mungu)
Smartdesmart
Ijumaa, Agosti 10, 2018
0
Alhamisi, 9 Agosti 2018
DUH KALALE MAHARAPEMA BABU YETU (NEVER SEE U AGAIN)
Smartdesmart
Alhamisi, Agosti 09, 2018
0
MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ leo Agost 9, 2018. Mzee King Majuto alifariki dunia jana majira ya saa 2:00 usiku Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Baada ya kuaga mwili utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa. Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
Jumatano, 8 Agosti 2018
MZEE MAJUTO 😭😭😭 AMEFARIKI DUNIA LEO TAREHE 8/08/2018 CHANZO CHA KIFO CHAKE NI
Smartdesmart
Jumatano, Agosti 08, 2018
0
MSANII nguli wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman ‘Mzee King Majuto’ amefariki dunia majira ya saa 2:00 usiku huu wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa. Mtoto wa marehemu aitwaye Abuu amethibitisha kifo cha baba yake. Pia, mchekeshaji Joti ndio wa kwanza kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa instagram. “R.I.P King Majuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana katika Tasnia ya Comedy Tanzania, sisi wanao, tutakukumbuka kwa kazi zako, upendo wako, tabasamu lako Daima milele, tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi, pumzika kwa Amani Mzee wetu,” amendika Joti. Mzee Majuto alizaliwa mwaka 1948 mkoani Tanga na kusoma Shule Msambwini, mkoani humo, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 10. Hivi karibuni Mzee Majuto alisafirishwa na kupelekwa nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejea nchini ambapo alipelekwa Muhimbili kuendelea na tiba yake. Mzee Majuto ndiye alikuwa muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC), alikuwa mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali. “Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un, We belong to God and to Him we shall return.”